Monday, February 16, 2015

Igoma mpaka Kisesa, Mwanza

Bustani nzuri katika kituo cha mafuta, Kisesa.

Biashara pembeni kabisa ya barabara kuu, Mwanza - Musoma. Hela na Uhai unachagua nini??

Maisha.

Jeneza lenye mwili wa Marehemu bibi Kisena likiwa kanisani kabla ya mazishi.
Jana tulimzika bibi Kisena, bibi niliyemfahamu kanisani kwetu kwa miaka kama minne hivi iliyopita. Amefariki akiwa na miaka 80 na hadi anafariki alikuwa ni mama ambaye kila mtu alimpenda.

Nimejifunza yafuatayo;

1. Penda kwa moyo wote. Na kama unampenda mtu umwambie usikae kimya. Unaweza ukachelewa.
2. Weka utaratibu wa kuwatembelea watu na jitahidi kuwafahamu. Huwezi kufahamu jinsi utakavyoyaathiri maisha yao.
3. Tabasamu kwa kila mtu hata kama humjui, itaifanya siku yake iwe nzuri.



Bibi kisena amemaliza kazi yake, amepumzika. Change today for tomorrow.

Sunday, February 15, 2015